HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 30, 2013

USAIN BOLT KUSHIRIKI DIAMOND LEAGUE JULAI 26 NA 27


Usain Bolt akionesha manjonjo yake wakati akishangilia kushinda tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka 'Laureus World Sports Award' aliyokabidhiwa mwezi uliopita baada ya kufanya vema mwaka jana 2012.

LONDON, England

MKALI wa mbio fupi duniani, Usain Bolt anaweza kuwa mmoja wa washiriki wa mbio za Diamond League ambazo ni sehemu ya London 2012 Anniversary zitakazofanyika Julai, baada ya wakala wa mchezaji huo kufichua "makubaliano chanya" yamefanyika.

Ni mbio za pili baada ya Olimpiki, kwani Bolt hajawahi kukimbia nchini Uingereza tangu mwaka 2009 kwa sababu ya sheria ya kodi inayolazimisha mgawo wa pato lake ama zawadi ya ushindi.

Hata hivyo, msamaha wa makato ya kodi kwa "wanamichezo wasio wazawa wa Uingereza" katika bajeti mpya imeondoa kikwazo hicho.

Mbio hizo za siku mbili za Diamond League zinatarajia kufanyika Ijumaa ya Julai 26 na Jumamosi Julai 27, ikifuatiwa na siku ya matukio ya michezo ya Paralimpiki.

Bolt nyota wa mbio fupi raia wa Marekani mwenye 26, alishinda dhahabu tatu katika Olimpiki ya kiangazi jijini London mwaka jana, akiweka rekodi katika mbio za mita 100 na kuwasaidia wenzake kubeba dhahabu ya mita 400 kupokezana vijiti.

Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo inatarajia nyota huyo atashiriki kwa ufanisi ikiwa ni sehemu yake ya kujiandaa na mbio za ubingwa wa Dunia zitakazokimbiwa jijini Moscow wiki mbili baadaye.

"Tuko katika makubaliano chanya ya mazuingumzo, ingawa bado kuna vitu havijakamilika," alisema wakala wa Bolt, Ricky Simms, kuiambia BBC Sport.

BBC Sport

No comments:

Post a Comment

Pages